Katibu Mkuu Umoja wa vijana taifa (UVCCM) Ndg. Kenani Kihongosi ameipongeza Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo kwa uwezeshaji mzuri kwa vikundi vya vijana kupitia mikopo ya 10% ya mapato ya ndani ambapo kupitia mikopo hiyo vijana wengi wanajipatia kipato na kuzalisha ajira kwa vijana wenzao.
Pongezi hizo amezitoa leo septemba 10, 2022 wakati alipotembelea kikundi cha vijana cha UMOJA NI NGUVU kilichopo katika halmashauri hiyo kata ya kibamba kinachojishughulisha na utengenezaji wa urembo wa nyumba kupitia unga wa gypsum na kueleza kuwa kutoa mikopo hiyo ni kutekeleza kwa vitendo dhamira ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha vijana wanawezeshwa.
Kenani amesema kuwa, Kwa mujibu wa taarifa ya kikundi hicho, Vijana hao baada ya kupata mkopo wa Halmashauri wa shilingi Milioni 37.5 wameboresha uzalishaji wa bidhaa za kiwanda chao, kuongeza wateja , kufanya marejesho kwa wakati na kulipa kodi za Halmashauri na TRA.
Kenani amekiri kuwa, Moja ya changamoto kubwa kwa vijana wanaopata mikopo hii hawafanyi marejesho lakini kikundi hicho kinafanya marejesho vizuri na wana mpango wa kumaliza mkopo wao kabla ya muda uliopangwa, “nawapongeza sana”.
“Vijana wakiwezeshwa wakafanya kazi za uzalishaji mali na biashara ni walipaji wazuri wa kodi za serikali na nchi itapiga hatua kubwa kimaendeleo” alieleza Kenani.
Aidha, amesema pamoja na mafanikio ya kikundi hicho ameitaka Halmashauri kuhakikisha vijana hao wanasaidiwa kutatua changamoto zao hasa ya kupata gari kwa ajili ya kusafirishia bidhaa zao kwa wateja “na hili najua lipo ndani ya uwezo wenu kupitia mapato yenu ya ndani, nimetembelea vikundi vingi sana lakini kikundi hiki kinaweza kuwa cha mfano katika kuitendea haki mikopo hii kupitia mapato ya ndani”
Wito wangu kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii ni kuendelea kutoa elimu kwa vijana namna ya kupata mikopo hii kwa kuwaelekeza vitu vya kuzingatia kwa ajili kupata mikopo hiyo ili tuwe na vijana wengi wanaojishughulisha na kutoa ajira kwa vijana wengine.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa