Kikao hicho cha Halmashauri kuu kimefanyika katika ukumbi wa LA DARIOT na kuongozwa na Mwenyekiti wa chama Wilaya ya Ubungo Ndg.Lucas Mgonja Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe.Kisare Makori na Kuhudhuriwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Beatrice Dominic Katibu Tawala wa Wilaya ya Ubungo James Mkumbo viongozi wa chama wilaya ya Ubungo na wataalam kutoka Manispaa ya hiyo na mashirika na wakala wa serikali wanaofanya kazi katika Wilaya hiyo.
Wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa Ilani kwa kipindi cha miaka mitano Mkuu wa Wilaya alipongeza ongezeko la mapato kwa 90% na kutumika kwa mfumo wa kietroniki wa kukusanyia mapato( POS machine).
Vilevile Halmashauri imefanikiwa kupata Hati safi kwa kipindi chote tangu 2016 mpaka 2020.
Pia sekta ya Afya imeimarika kwa upatikanaji wa dawa na chanjo ya watoto chini ya miaka mitano na Utekelezaji wa miradi ya Afya mfano ujenzi wa zahanati ya Kibamba, kituo cha Afya Kimara na *"Nitoe shukrani kwa Mhe.Rais Dk. John Pombe Magufuri kwa kusaidia katika kuhakikisha Wilaya ya Ubungo inapata hospitali ya Wilaya."* Aliongeza Mkuu wa Wilaya.
Pia Usambazaji wa maji umefanikiwa kwa kiasi kikubwa kutoka 55% mpaka 80% zaidi kwa wananchi wa Wilaya ya Ubungo ambao maeneo yao yalikuwa na changamoto ya upatikanaji wa maji.
Nitoe pongezi pia kwa Sekta ya Maendeleo ya Jamii kwa kuwawezesha vikundi vya vijana, walemavu na wanawake kufikia malengo yao na kupewa elimu ya ujasiriamali kwa vikundi 788.
Nipongeze pia kwa sekta ya Ustawi wa jamii kwa kufanikiwa kutoa vitambulisho vya msamaha wa kupata matibabu kwa wazee 13,446, vikundi 33 vya walemavu wamepatiwa mikopo pia.
Pia Sekta ya Mipangomiji kwa ulipaji wa fidia eneo la Mbezi Luis, kufanya uthamini wa maeneo mapya kama kibesa n.k na kwa sekta nyingine kama Teknolojia ya Habari na Uhusiano, sekta ya kilimo, ushirika,sekta ya Mifugo, Tarula, Dawasco, sekta ya Elimu msingi na sekondari, sekta ya Utamaduni na Michezo niwapongeze pia kwa utekelezaji mzuri wa shughuli za kimaendeleo.
Mkuu wa Wilaya alishukuru kwa uongozi wa chama kwa ushirikiano wao kwa kipindi chote pamoja na Mkurugenzi na timu nzima ya Wataalam.
Wakati anafunga kikao Mwenyekiti wa CCM Wilaya alimpongeza Mkuu wa Wilaya na uongozi mzima wa wataalam kutoka Manispaa ukiongozwa na Mkurugenzi kwa kazi nzuri zinazofanyika kwa ajili ya wananchi wa Ubungo na utekelezaji mzuri wa miradi.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa