Maafisa wa Serikali wasisitizwa kutoa elimu kwa wafanyabiashara wanapofanya ukaguzi kabla ya kutoza "fine" ili kuboresha, kukuza na kuleta maendeleo na ushirikiano baina ya wafanyabiashara na wataalam.
Akizungumza katika baraza hilo Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mheshimiwa Kheri James Leo tarehe 14 julai, 2022 amesisitiza Lengo la kikao hicho ni kujadili maswala yenye tija na manufaa yatakayoleta maendeleo kwa kuboresha na kukuza biashara katika Wilaya hiyo
Aidha Kheri amesema kuwa jukumu la kamati ya ulinzi na usalama ni kulinda amani, kwa kuzingatia hilo tutasaidiana na nyie wafanyabiashara kutatua changamoto mbalimbali na kukuza swala la usalama kwa wafanyabiashara
Aidha, Nisisitize kwa Wanaofanya maegesho ya mabasi katika maeneo ambayo sio rasmi kwa kupakia abiria ni lazima hatua zichukuliwe kwani ni kinyume Cha Sheria
"Wananchi waendelea kukumbushwa kuzingatia stendi ambazo ni rasmi kwaajili ya kupata usafiri na sio vyinginevyo na wale wanaopakia na kushusha sehemu ambazo sio rasmi watachukuliwa hatua na kuagizwa kuacha Mara moja" amesisitiza kheri
Nae mjumbe wa baraza la biashara kutoka TABOA Mustapha Mwalongo ameishukuru Manispaa ya Ubungo kwa kuendelea kuboresha mahusiano mazuri na hasa katika kusikiliza kero zao na kuzifanyia kazi
Sambamba na hayo wajumbe waliendelea kuishukuru Manispaa ya Ubungo kwa kuendelea kusikiliza na kutatua changamoto wanazokutana Kama wafanyabiashara wanapokuwa katika maeneo yao ya biashara
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa