Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo tarehe 31/1/ 2020 imefanya kikao kazi katika ukumbi wa LA DARIOT uliopo Mbezi na watumishi wote na wadau wa Manispaa kufanya tathmini ya utendaji kazi wa miezi sita (Kuanzia Julai hadi Disemba 2019).
Katika kikao hicho mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa wilaya ya Ubungo Mhe.Kisare Makori na aliongozana na Meya wa Manispaa ya Ubungo Mhe Boniface Jacob pamoja na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Beatrice Dominic na kamati ya Ulinzi ya Wilaya.
Wakati akifungua kikao hicho Mkuu wa wilaya ya Ubungo Mhe. Kisare Makori alitoa pongezi kwa Manispaa ya Ubungo kwa maendeleo ambayo yanaendelea kufanyika katika Manispaa na kwa kitu walicho kifanya leo cha kuandaa kikao kazi kwa watumishi wote wa Halmshauri na kutoa pongezi kwa nafasi ambayo imepata kwa watoto wanaojiunga na kidato cha kwanza kupewa kipaumbele katika kuingia kidato cha kwanza.
Aidha Mkuu wa Wilaya aliongelea ukamilishaji wa miradi mbalimbali kwa wakati, kujua na kuzingatia thamani ya miradi, uzingatiaji wa sheria."Nipende kuwakumbusha mambo muhimu ambayo Rais wetu wa awamu ya tano anataka tuyafanye na kuyazingatia hasa Utawala bora wenye usimamizi mzuri wa miradi na kufanya yale ambayo tunapaswa kuzingatia kama watumishi, na pia suala la rushwa ni kitu ambacho kinapigwa vita na Serikali ya awamu awamu ya tano. alisema DC.
Nae Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo aliiwasilisha bajeti ya mwaka 2020/2021 ya Manispaa na kuonyesha miradi mbalimbali ambayo inafanyika na kutekelezwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.
"Kama Halmashauri tunategemea kununua mashine 100 za kukusanyia mapato ambazo tutaanza nazo. Na jambo ambalo tuna changamoto nalo ni uwepo wa Ofisi ya kudumu kwani ambayo inatumika kwa sasa ni jengo la muda inasababisha watumishi kutokua sehemu moja kutokana na jengo tunalotumia kuwa dogo lakini ujenzi wa jengo la Manispaa la kudumu bado unaendelea.Pia nipende kuwa karibisha katika vituo vya afya vilivyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo vituo vyetu viko vizuri na huduma zinazotolewa ni za uhakika." Aliongeza Mkurugenzi
Aidha Halmashauri ilitoa vyeti kwa baadhi ya kampuni kwa kutambua mchango wao kwenye kusaidia kusukuma maendeleo ya Wilaya.
Kwa kufunga Mkurugenzi aliwashukuru wageni wote kwa ujio wao na kuwakaribisha Manispaa ya Ubungo.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa