Manispaa ya Ubungo kupitia Idara ya Maendeleo ya Jamii wamekabidhi bajaji 10 zenye thamani ya shilingi Milioni 86 kwa kikundi cha UMOJA WA MADEREVA BAJAJI UBUNGO kinachofanya shughuli zake Mbezi Magufuli Bus Terminal.
Akikabidhi bajaji hizo Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mheshimiwa Kheri James amesisitiza nidhamu ya fedha iweze kutumika itakayo wawezesha kufanya marejesho ya fedha hizo kwa wakati.
Aliendelea kwa kusema kuwa "Raha yetu na matumaini yetu ni mkaajili na vijana wengine na pia mkamiliki biashara nyingine".
Niwapongeze mmekuwa kikundi cha mfano mmefanya vyema marejesho ya fedha mlizopokea awali na mkafanikiwa kupata kiasi kikubwa zaidi na leo hii mmepata bajaji kaendeleeni kuwa chachu kwa vijana wengine. Alisema Kheri.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa