Wakulima Wadogo Wilaya ya Ubungo wamepewa elimu Kuhusu kilimo Cha Mchicha kwa Lengo la kuwaongezea ujuzi katika kuboresha maendeleo ya zao hilo
Mafunzo hayo yametolewa tarehe 8.10.2021 katika Kituo Cha Mafunzo kwa wakulima vijana Cha Kibamba Youth Agripreneur kilichopo Kibamba
Akiongea wakati wa mafunzo hayo elekezi kwa wakulima Mbunge wa Jimbo la Kibamba Issa Mtemvu amekipongeza kikundi Cha vijana wa Kibamba youth agripreneur kwa kilimo na ufugaji wakisasa wanachofanya
Nimefurahishwa na kilimo Cha mchicha ambacho nimekikuta hapa, sikutegemea kuona kilimo hichi naikawe fursa kwa vijana wengine.Alieleza Mtemvu
"Mtemvu aliendelea kusema kuwa fursa hii imetolewa kwenu wakulima mkaifanyie kazi namnapofika kwa wakulima wengine ambao wako mitaani mkawape elimu hii ambayo itawaisaidia na wao"
Aliendelea kusisitiza kilimo ni tija na Chachu ya maendeleo na ni fursa kubwa tujielekeze katika kilimo kinamanufaa makubwa hata katika ujenzi wa taifa
Nae Dk.Minja Mtafiti kutoka taasisi ya TARI( Tanzania Agricultural Research Information) Mikocheni amesisitiza wakulima Kutumia kilimo bora na Cha kisasa kwa kutumia mbegu Bora tano za mchicha ambazo ni Pori,madira 1 , madira 2, Nguruma na Akeri ambazo zitaendelea kusambazwa katika maeneo mbalimbali ya maghara ya mazao na kutumika
"Nipendelee kuwashauri kutumia Mchicha kwani ni lishe bora kwa afya na uimarisha mwili kwa vitamini" alisema hayo Dk.Minja
Aidha Afisa kilimo,Ushirika na umwagiliaji Manispaa ya Ubungo Happiness Mbelle amemshukuru Mgeni rasmi nakueleza jitihada ambazo halmashauri inafanya ilikuendeleza kilimo Cha vijana wa Kibamba youth Agripreneur kwa kuwapatia eneo la hekari 2 katika shamba la Kibesa ambalo linamilikiwa na Halmashauri hiyo
Akishukuru kwa niaba ya wakulima Ester Swebe ameeleza manufaa aliyoyapata kutokana na kilimo na kuwashukuru wawezeshaji waliotoa elimu kuhusiana na zao la mchicha na pia kuwapongeza maafisa ugani wa Manispaa kwa juhudi za kutoa elimu kwa wakulima wadogo
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa