Vijana wametakiwa kuchangamkia fursa katika sekta ya kilimo kujiajiri na kujikwamua kiuchumi badala ya kutegemea kuajiriwa pekee
Kauli hiyo imetolewa na wajumbe wa kamati ya Uchumi, Elimu na Afya ya Manispaa ya Ubungo walipotembelea na kukagua mradi wa shamba darasa lililopo Kibesa kata ya mbezi ambapo serikali imewekeza miundombinu kwa ajili ya kuwezesha vijana kulima mazao mbalimbali kwa njia ya umwagiliaji.
Akiongea wakati wa ukaguzi wa mradi huo, mwenyekiti wa kamati hiyo Edward Lazier Mhe. Diwani kata ya Saranga amesema kwa kutumia eneo hilo vijana wa ubungo wananwaweza kufanya uzalishaji wa mazao mbalimbali ya kilimo kwa njia za kisasa na wakajipatia kipato badala ya kukaa kusuburi kuajiriwa.
Katika mradi huo, Halmashauri imewekeza miundombinu ya maji, kutwaa ardhi na ujenzi kwa kitalu nyumba kupitia fedha za ofisi ya waziri mkuu ambapo vijana 100 wamepata mafunzo ya kutengeneza kitalu nyumba na uzalishaji kupitia kitalu hicho, kazi iliyobaki ni vijana kuona umuhimu wa kujiajiri kupitia kilimo ambacho kinamahitaji makubwa sokoni.
Aidha, Laizer amesema zaidi ya milioni 350 zimewekezwa katika eneo hili ambapo milioni 300 zimelipia fidia ya ardhi ekari 28, milioni 32 kuchimba kisima na miundombinu yake na milioni 20 kutoka ofisi ya waziri mkuu zimetumika kujenga Kitalu nyumba ni muhimu eneo hili likawa kituo cha uzalisjhaji kwa kufanya uwekezaji mkubwa zaidi kwa kulima mazao mbalimbali ili wananchi wajifunze kwa vitendo.
Kwa umape wake Hamisi Hassan mmoja wa vijana wanaonufaika na mradi huo ameishukuru serikali na ofisi ya waziri mkuu kwa kuwezesha vijana kupitia sekta ya kilimo ili wajiajiri badala ya kusuburi kuajiriwa na serikali kwani kilimo kinalipa
Hamisi amesema kuwa “wito wangu kwa vijana ni kudhubutu kuanza kulima kwani mahitaji ya mazao ya chakula ni makubwa sana, mfano kwenye kitalu nyumba hiki tunazalisha hoho za rangi nyekundu na njano na soko lake ni kubwa na zinauzwa bei nzuri sana,”
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa