Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo leo imezindua chumba cha Upasuaji katika Kituo chake cha Afya cha KIMARA kwa kufanya upasuaji wa mama mjamzito na kwa mafanikio makubwa mama amepata mtoto akiwa salama. Upasuaji huo ulifanyika chini ya Uongozi wa Mganga Mkuu wa Manispaa ya Ubungo Dkt.PETER NSANYA na kufanikiwa kumpata mtoto wa kike mwenye uzito wa kilo 2.6.
Kabla ya upasuaji huo Mama huyo Bi. Siajabu Zawadi Mshauri alishawahi kufanyiwa upasuaji wa aina hiyo mara mbili katika Hospitali ya Taifa Muhimbili. Na hali ya Mama na Mtoto inaendelea vizuri.
Nae mama mzazi wa mtoto huyo Bi. SIAJABU ZAWADI MSHAURI amewashukuru madaktari na kufurahia kupata mtoto wa kike.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa