Mkuu wa Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika Happiness Mbelle amepokea ugeni wa wanafunzi kutoka chuo cha Maji (Water Institute) waliokuja kujifunza teknolojia ya kilimo cha umwagiliaji kwa njia ya matone(Drip Irrigation).
Kituo hicho kina eneo la ukubwa wa ekari 28 lililopo Kata ya Mbezi Mtaa wa Mpigi Magohe eneo la Kibesa na jumla ya Vikundi vitatu 3 vya vijana ambavyo ni Youth Confiderative versus poverty, kikundi cha Vijana wakulima Mapambano kilichopo kata ya Mbezi (kibesa) na kikundi cha vijana shupavu kutoka Kata ya Kibamba ambavyo vimefanikiwa kuanza uzalishaji katika eneo husika.
Aidha vikundi hivyo vilipata mkopo wa 10℅ kutoka katika mfuko wa vijana na walemavu kupitia Idara ya maendeleo ya jamii na vimefanikiwa kuzalisha mazao mbalimbali kama (mahindi,miogo,viazi,hoho,bamia n.k)
Halmashauri imeendelea kushirikiana na wadau wa kilimo IITA katika kuhakikisha vikundi vinapata elimu bora,msaada wa pembe jeo na elimu ya kanuni bora za kilimo ili kuhakikisha wanazalisha kwa tija ilikufikia uchumi wa kati wa viwanda. Alisema hayo Happiness Mbelle
"Pia kupitia mradi huo taasisi mbalimbali zimeshawishika kuja kujifunza na mikakati iliopo ni kujenga nyumba ya kijani(Green house), visima na majengo yatakayotumika kama madarasa ya kufundishia wakulima na kutengeneza jengo la usindikaji (Agricultural Processing Industry) ili kuongeza thamani ya mazao yanayozalishwa" Aliongezea Happiness Mbelle
Tunaendelea kuomba wadau na mtu mmoja mmoja wanaotuzunguka kutoa ushirikiano ili tufikie malengo. "Sambamba na hilo Happiness Mbelle alisema kuwa mradi una changamoto kubwa ya maji"
Nae mshauri wa wanafunzi kutoka chuo cha maji Ndg.Alistides Alfred alishukuru kwa elimu ambayo wanafunzi wameipata kutoka kwa Afisa Kilimo wa Manispaa kwani imeongeza ufanisi na imewajenga wanafunzi kitaaluma zaidi na kuhaidi kushirikiana na Afisa Kilimo bega kwa bega katika kuhakikisha tatizo la maji linatatuliwa kwa kupitia wataalam kutoka katika chuo hicho.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa