Shirika lisilo la kiserikali linalofanya shughuli za ulinzi na uhifadhi wa mazingira na rasilimali za maliasili la Lawyers Environment action team (LEAT) limetembelea Kata ya Kimara mtaa wa mavurunza uliopo Wilaya ya Ubungo kujionea mazingira korofi
Aidha wakati wakitembelea katika mtaa wa mavurunza wananchi walielezea changamoto wanazozipata kutokana na mto huo kupita katika nyumba za watu na hata nyumba nyingine kusombwa na maji na kupelekea hali hatarishi kwa wakazi waliobaki na watoto wa shule kwenda mashuleni wakati wa mvua.
Akizungumza na wataalam kutoka LEAT diwani wa kata hiyo Mhe.Nuru Mbezi aliomba shirika hilo kwa kushirikiana na serikali kusaidia namna bora ya kutatua changamoto hiyo kwa wakazi wa mavurunza ili kuleta ahueni ya eneo hilo korofi kwa jamii kwaajili ya kuleta ustawi wa afya ya mazingira.
Aliendelea kwa kusema kuwa wanakijiji wa eneo hilo wanachukua hatua mbalimbali katika kudhibiti maji kusogea katika maeneo yao lakini jitihada zimekuwa zikifeli hata kupelekea mto huo kuendelea kusogea.
Sambamba na hayo Afisa mazingira Manispaa ya Ubungo Ndg.Ezra Guya aliomba wananchi kuzingatia pia sheria za mazingira hasa katika ujenzi wa maeneo yaliyohatarishi karibu na mito kwa kuhakikisha wanajenga nyumba zao umbali wa mita 60 kutoka katika mito hiyo
Pia Wananchi waeneo hilo waliomba serikali kuliangalia jambo hilo kwa kina zaidi na kuweza kuwasaidia kupata msaada wa kujengewa daraja iliwaweze kufanya shughuli zao hata kipindi cha mvua.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa