Asasi isiyokuwa ya kiserikali inayofanya shughuli za ulinzi na uhifadhi wa mazingira na rasilimali ya Lawayers Environment Action Team (LEAT) tarehe 16/3/2021 katika ukumbi wa Green View Hotel uliopo Shekilngo limetoa mafunzo kwa watendaji wa Kata,Mitaa, Maafisa Afya, Maafisa Mazingira, Wenyeviti wa Mitaa,maafisa Masoko, Machinga na Mama lishe juu ya namna bora ya kutunza mazingira.
Lengo la kutolewa kwa mafunzo hayo ni kuwajengea uzoefu na kuwapa ufanisi zaidi kuhusiana na utunzaji wa mazingira na kukabiliana na changamoto za kimazingira na namna bora ya kutunza mazingira
Aidha katika kuhakikisha mazingira yanakuwa safi na salama LEAT imeendelea kusisitiza kwa changamoto zozote za kimazingira na msaada wa kisheria itaendelea kutoa ushirikiano kwa Manispaa ya ubungo na kuhamasisha zaidi watendaji wa kata, mitaa na maafisa afya na mama lishe kuendelea kuboresha mazingira na kuhakikisha utunzaji wa mazingira katika maeneo yao
Pia LEAT wameendelea kusisitiza mikakati ya utunzaji na udhibiti wa taka ngumu na taka miminika zinahifadhiwa mahala sahihi ilikuepusha uchafuzi wa mazingira na hata maafisa mazingira kuhakikisha wanakuwa mstari wa mbele kuondoa taka katika maeneo yasiyo rafiki
Nae mama lishe Suzana Elias ameishukuru LEAT kwa mafunzo hayo kwa kuweza kuwakumbusha na kuwaongezea uwezo wa kwenda kufanya mazingira ya biashara kuwa safi na salama kwa ustawi wa afya kwaajili ya wateja wao
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa