Kuelekea kilele Cha maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani tarehe 5.6.2022 , Manispaa ya Ubungo Leo tarehe 4.6.2022 kwa kushirikiana na wadau wa Songas , Twaweza na Roots and Shoots imeadhimisha siku ya mazingira Duniani kwa kupanda miti 500 katika eneo la jengo la utawala lililopo luguruni pamoja na kufanya usafi.
Akifungua Maadhimisho yaliyoenda sambamba na Kauli mbiu ya TANZANIA NI MOJA TU , TUNZA MAZINGIRA. Afisa Tarafa Beatrice Mbawala amesema kuwa zoezi hili ni endelevu na Kila mwananchi katika Wilaya ya Ubungo ahakikishe anafanya usafi katika maeneo yote yaliyowazunguka
Aidha kaimu Mkurugenzi Dkt. Peter Nsanya amesisitiza swala la upandaji wa miti katika maeneo yetu kwa kuwahamasisha wananchi wa Wilaya ya Ubungo ili kuweka mazingira Safi na salama
"Niwashukuru wadau wote walioshiriki katika zoezi hili na tuendelee na utamaduni huu wa kupanda miti na kusafisha mazingira" alieleza Nsanya
Halikadhalika, kaimu Mkuu wa idara ya mazingira Nice Vahaye amesema kuwa zoezi hili ni endelevu kwa Manispaa ya Ubungo na elimu imekua ikitolewa kwa jamii kuhusiana na upandaji miti sambamba na sheria ambazo zinawahimiza wananchi wote kuendelea kutunza mazingira
Nae Meneja wa Songas tawi la Ubungo dkt. Michael Mngodo ameshukuru Manispaa ya Ubungo kwa kushirikiana kikamilifu katika kuboresha Hali ya mazingira kwa kufanya usafi na kupanda miti na kuahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Manispaa ya ubungo
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa