Manispaa ya Ubungo kwa kushirikiana na wadau wa mazingira wakiwemo, Nipe Fagio, Roots & Shoots, HUDEFO, Zaidi Recyclers, Forum CC imeazimisha siku ya usafi duniani kwa kufanya usafi Eneo la Mbezi Luis (Upande wa Kata ya Msigani na Kata ya Mbezi).
Akiongea Afisa Afya wa Manispaa hiyo Bw. Boniface Katikiro ametoa shukrani kwa wananchi pamoja na wadau waliojitokeza kushiriki usafi huo, ambapo ametoa wito kwa wananchi na wadau mbalimbali kuendelea kujitokeza kushiriki usafi wa mazingira wa kila mwisho wa mwezi na kuhakikisha mazingira yao ya makazi na biashara yanakuwa safi muda wote.
“Mbezi ni lango la Jiji taswira ya Dar es salaam inaanza kuonekana Mbezi hivyo ni vyema mazingira haya kuwa safi muda wote” Alisema Katikiro.
Kwa upande wake Community Mobilization Officer wa Nipe Fagio Bi. Nasra Juma ameeleza lengo la maazimisho hayo ni kuhamasisha jamii juu ya umuhimu wa kufanya usafi wao wenyewe kwenye maeneo yao.
Aidha, Nasra ametoa wito kwa Jamii kuacha matumizi ya mifuko ya plastiki za maramoja ili kuendelea kutunza mazingira kutokana na athari ambazo zimekuwa zikielezwa juu ya mifuko hiyo
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa