Maafisa biashara Manispaa ya Ubungo wakiongozwa na Afisa Biashara wa Manispaa Prisca Mjema tarehe 5/5/2020 wamefanya ziara ya kukagua usambazaji wa sukari katika magodauni na maduka ya jumla yaliyopo Wilaya ya Ubungo.
Wakati wa ziara hiyo walitembelea Kata ya Manzese na Kata ya Makurumla ili kujionea hali halisi
Aidha walitembelea katika magodauni 13 na maduka ya jumla 20 ambayo walifanikiwa kupata godauni moja la bwana Khamis Mohamed Salehe aliyekuwa akiuza kg50 kwa Tsh laki 129,000 na kufanikiwa kumpa bei elekezi ambayo Serikali imepanga ya Tsh laki 127,000.
Hivyo wamewaasa wauzaji wa jumla na wamiliki wa Magodauni kuhakikisha wanafuata sheria iliyowekwa na Serikali ili kuepukana na athari nyingine mbalimbali
NB.kwa atakaekwenda kinyume na maagizo ya serikali atachukuliwa hatua kali za kisheria.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa