Siku 1000 katika maisha ya mwanadamu ni muhimu sana, Kila mwanamke anatakiwa kuzingatia anapata lishe Bora pale tu anapojijua ni mjamzito ili kupata mtoto asiyekuwa na udumavu wala changamoto yoyote ya kiafya
Hayo yameelezwa Leo tarehe 13 Januari 2023 na Afisa lishe Manispaa ya ubungo Beatrice Mossile alipokuwa anatoa elimu kuhusu maswala ya lishe kwa maafisa maendeleo na Tasaf Manispaa ya ubungo ili waweze kutoa elimu hiyo katika ngazi ya jamii
Ni muhimu mama kuhakikisha anakula mlo kamili anapojijua ni mjamzito na kuzingatia anapata madini ya chuma ili kuepusha kupata watoto wenye Afya dhaifu, vifo vya watoto wachanga na hata kupoteza maisha wanapojifungua. Alieleza hayo Mossile
Aliendelea kwa kusema kuwa ni muhimu kuelimishe jamii kuhusu kula Mlo kamili kwa kuzingatia makundi matano, kundi la kwanza ni vyakula vya nafaka, mizizi na ndizi mbichi, kundi la pili ni mimea na wanyama, la tatu ni mbogamboga, la nne ni matunda na la tano ni mafuta na sukari
Aidha, Mossile aliendelea kuwakumbusha wakina mama wote pale tu unapojihisi ni mjamzito Kuhudhuria kliniki ni muhimu sana hii kumlinda mtoto aliye tumboni kwani unapowai kufika katika kituo cha Afya inasaidia kupata huduma za Afya ya uzazi mapema ambapo itasaidia katika ukuaji wa watoto na kusaidia kuzaliwa wakiwa na Afya nzuri
Uzingatiaji na ulaji wa vyakula vyenye ubora kwa Afya husaidia kuepukana na magonjwa yasiyoambukiza na hata kuweka mwili kuwa imara
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa