Shirika lisilo la kiserikali la Lawyers Environment Action Team (LEAT) kwa kushirikiana na Manispaa ya Ubungo wamejipanga Kuja na mkakati wa kuhakikisha wanawajengea uwezo wataalam wa Mazingira ngazi ya kata kukabiliana na changamoto za kimazingira zinazotokea katika kata zao ikiwa ni moja ya mkakati wa kupunguza athari za kimazingira kwa wananchi.
Mkakati huo ulielezwa na Afisa Mazingira wa Manispaa ya Ubungo Ezra Guya Wakati wa ziara iliyofanyika tarehe 14/6/2021 ya kutembelea maeneo ya Ubungo Kisiwani na Kibo yaliyopitiwa na Mto Gide ambao unasababisha maafa kwa wananchi ikiwemo nyumba kubomoka, watu kushindwa kuvuka na uhalibifu wa Mazingira kwa ujumla
" Kila afisa mazingira kwenye kata yake anatakiwa kuwaelimisha wananchi wapande miti, kutokutiririsha maji machafu kwenye mito na kutokutupa taka ili kutunza mazingira na pia kuepusha milipuko ya magonjwa yatokanayo na uchafu" alieleza Guya
Aidha, Guya aliwakumbusha wananchi kuzingatia Sheria ya kujenga makazi umbali wa mita 60 kutoka mtoni ilikuepusha madhara ya mafuriko na kubomolewa nyumba zao
" Ikumbukwe kuwa moja ya maeneo ambayo wananchi wana athiriwa na mafuriko kipindi cha mvua ni yale yaliyo karibu na mito hivyo zingatieni kanuni ya kujenga umbali wa mita 60" alifafanua Ezra
Katika kuunga juhudi za Manispaa ya kukabiliana na changamoto za mazingira, Asasi ya LEAT imeahidi kushirikiana na Manispaa katika kutatua changamoto za mazingira katika maeneo mbalimbali ikiwemo kwenye masoko,mito na maeneo mengine ilikuhakikisha mazingira yanakuwa safi.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa