Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Beatrice Dominic leo tarehe 2 septemba,2021 amefungua mafunzo elekezi kwa maafisa Ugani yaliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Manispaa hiyo yenye lengo la kuwaongezea ujuzi na ustadi Kuhusuana na mfumo wa MOBILE- KILIMO (M-kilimo) teknolojia ya kutumia simu ambao unalenga kusaidia wakulima,wafugaji na wavuvi kuyafikia masoko ya mazao kwa njia ya simu
Akiongea wakati wa kufungua mafunzo hayo Beatrice amewataka maafisa Ugani hao kuhakikisha kila mmoja wao anazingatia mafunzo hayo na baada ya kuwezeshwa waweze kujengea uwezo Kaya 10 kuhusuana na maswala ya kilimo
"Ni Fursa kwenu Kama maafisa Ugani wa mjini kuhamasisha kilimo hata Cha mbogamboga Katika Kaya ili kilimo kiweze kuendelea na kukua" alielezea Beatrice
Aidha muwezeshaji kutoka Katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Omari Rajabu ameelezea mchango wa kilimo kwa taifa ikiwemo kuongeza Pato la taifa 26.9% , ajira 58.1%, chakula Cha taifa 100%
Aliendelea kwa kuwajengea uwezo wataalam hao namna sahihi kutumia mfumo huo wa M-kilimo
Nae Mkuu wa Idara ya kilimo,umwagiliaji na ushirika Manispaa ya Ubungo Happiness Mbelle amemshukuru muwezeshaji na kuwataka maafisa Ugani kuzingatia mafunzo hayo na kuhakikisha wanayafanyia kazi hasa Katika swala la matumizi ya mfumo yatayochochea tija Katika sekta ya kilimo
N.B Mafunzo hayo elekezi yaliyoanza leo yatakafanyika kwa muda wa siku mbili na kumalizika kesho tarehe 3,septemb,2021
Attachments area
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa