Maafisa ugani Manispaa ya Ubungo wapatiwa mafunzo ya kutumia mfumo wa kieletroniki wa Mobile Kilimo(M-Kilimo) wa Wizara ya Kilimo unaotoa huduma za ughani na masoko kwa wakulima,wavuvi na wadau mbalimbali wa sekta ya Kilimo kwa kutumia simu ya mkononi.
Mafunzo hayo yamefanyika tarehe 25/3/2021 katika ukumbi wa mikutano uliopo Manispaa ya Ubungo- luguruni jijini Dar es salaam ukihusisha maafisa kilimo walioko ngazi ya Kata na makao makuu
Lengo la mafunzo hayo ni kutatua changamoto ya uhaba wa maafisa ugani na kutatua changamoto ya upatikanaji wa masoko ya mazao ya kilimo, mifugo na pia kuwaunganisha wakulima,wafugaji, wavuvi na wadau wengine wa sekta ya kilimo
Aidha muwezeshaji kutoka wizara ya kilimo Ndg.Rajabu Omary alisisitiza mafunzo hayo yanafaida kwa maafisa ugani kwani hurahisisha mawasiliano kati yao na mkulima,mfugaji na mvuvi na husaidia wakulima na wafugaji kuyafikia masoko ya mazao kwa urahisi pia kuwaunganisha wakulima,wafugaji,wavuvi na wadau wa Sekta ya kilimo katika mnyororo wa thamani
Sambamba na hayo Mobile Kilimo(M-Kilimo) ni jukwaa la mawasiliano linalowaunganisha wakulima,wafugaji,wavuvi na maafisa ughani kwa njia ya ujumbe mfupi wa simu vilevile jukwaa hili linawezesha wafugaji,wakulima, wavuvi na wafanya biashara mbalimbali kutangaza biashara na kutafuta masoko kwa kutumia simu ya mkononi
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa