Manispaa ya Ubungo kupitia Idara ya Afya na Ustawi wa Jamii imefanikiwa kutoa huduma ya afya ya akili na msaada wa kisaikolojia kwa kutoa elimu kwa wasafiri 73, jumla ya watu 33 masokoni , na pia kutoa msaada kwa watu 12 ambao ni wahanga wa UVIKO – 19.
Akiwasilisha taarifa hiyo katika kikao kilichofanyika tarehe 15/12/2021, Afisa Ustawi wa Manispaa ya Ubungo Zainabu Masilamba ameeleza kuwa wamefanikiwa kutoa elimu ya kujikinga na ugonjwa wa UVIKO - 19 kwa wamiliki 605 wa vituo vya kulelea watoto wadogo mchana (Day Care Centers) kwa kipindi cha kuanzia Machi, 2020 hadi Novemba, 2021.
Aliendelea kwa kuwasilisha taarifa ya mafanikio na mikakati ambayo itaendeleapo kutekelezwa kwa ajili ya kutoa huduma kwa watu na makundi maalum hasa yanayohusu maswala ya kupinga ukatili wa wanawake na watoto pamoja na kuwalinda na UVIKO-19.
Aidha alielezea moja ya mikakati yao ni kuendelea kufanya kazi bega kwa bega na Wadau na kuendelea kutoa elimu kwa jamii kuhusu kuchukua tahadhali ya kujikinga na UVIKO 19 ikiwa ni pamoja na kuchanja chanjo yake.
Nae Afisa Kilimo Manispaa ya Ubungo Stella Nzelu alitoa elimu ya uzingatiaji wa lishe bora ikiwa ni njia mojawapo ya kujikinga na UVIKO - 19 kwani lishe inasaidia kujenga kinga ya mwili na hivyo kusaidia kupambana na UVIKO - 19.
Pia Afisa Afya wa Manispaa ya Ubungo Iqbal Janja ameelezea kuwa wao wameweza kufanikiwa kwa kuhakikisha kuwa kila mwananchi anapata elimu ya kujikinga na UVIKO-19 lakini pia kuendelea kuhakikisha wananchi waendelea kupata chanjo na wameweza kwenda kwenye mikusanyiko ya watu na kutoa elimu ya kujikinga na UVIKO-19 na kushawishi kuchanja chanjo ya UVIKO-19.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa