Manispaa ya Ubungo leo tarehe 26/11/2022 imeadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia yenye kauli mbiu isemayo ‘’kila uhai una thamani tokomeza mauaji na ukatili dhidi ya wanawake na watoto’’
Maadhimisho hayo yalienda sambamba na maandamano yaliyoanza katika kituo kikuu cha mabasi cha Magufuli bus terminal hadi ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa hiyo na kupokelewa na Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo.
Maandamano hayo yamehusisha wadau mbalimbali wa ASAS za kiraia “NGOs” wakiwemo, vikundi vya wajasiriamali viliyopata mikopo ya asilimia 10 ya fedha za mapato ya ndani ya Halmashauri, SMAUJATA, wananchi, viongozi na wataalamu wa Manispaa hiyo.
Akiongea katika maadhimisho hayo Bi Hilda Malosha mratibu wa kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto wa wilaya hiyo amesema Manispaa imejipanga kupambana na ukatili wa kijinsia kwa kuanza kupita kwenye mitaa na kata kwa maeneo yote ya Magulio, vituo vya usafiri na nyumba za ibada kwaajili ya kutoa elimu ya kupinga ukatili wa kijinsia.
Malosha ameendelea kueleza maswala ya ukatili wa kijinsia yanaleta madhara makubwa katika jamii yasipo shughulikiwa ipasavyo, kila mwana jamii anawajibu wa kuhakikisha ukatili wa kijinsia unatokomezwa kwa kutoa taarifa kwenye vyombo husika kwa hatua zaidi.
Nae Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo Mhe. Jaffery Nyaigesha ameendelea kusisitiza kuwa ukatili wa kijinsia hautafumbiwa macho na yeyote atakaye bainika kufanya ukatili huo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake na ametoa wito kwa jamii kuhakikisha kila mmoja anawajibika kupinga ukatili wa kijinsia.
Kwa upande wake Bi. Elionora Joseph Mosha katibu wa Red Cross tawi la chuo kikuu cha Dar es Salaam ambae ni mmoja kati ya waandamanaji hao amesema ukatili wa kijinsia ni moja kati ya vitu vinavyopelekea mipango na ndoto za watu wengi hususani wanawake na watoto kushindwa kufikia ndoto zao hivyo ameiasa jamii kuacha vitendo vya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa