kila mwaka tarehe 1 disemba ni siku ya UKIMWI duniani ambapo maadhimisho hayo kitaifa yamefanyika mkoani Lindi na kwa mkoa wa Dar es Salaam yamefanyika katika halmashauri ya manispaa ya Temeke-Mbagala ambapo yamehudhuriwa na wananchi mbalimbali na vikundi vya kijamii pia yalienda sambamba na upimaji wa afya kwa wananchi.
katika maadhimisho hayo mgeni rasmi alikuwa kaimu mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya ilala Mhe Ng'wilabuzu Ndatwa Ludigija na wakuu wengine wa wilaya, wakurugenzi na wakuu wa idara kutoka katika manispaa hizo.
mganga mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Dkt Rashid Mfaume alitoa takwimu ya hali ya maambukizi kwa mkoa wa Dar es Salaam na jitihada zinazoendelea katika kupambana na maambukizi. alisema katika mkoa wa Dar es Salaam maambukizi ni asilimia 4.7 ikiwa ni sawa na uwiano wa watu wanne wenye maambikizi katika watu mia na kusema wanaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kupambana na maambukizi.
kaimu mkuu wa mkoa Mhe Ng'wilabuzu Ndatwa Ludigija alisema kwa niaba ya serikali kwa kushirikiana na asasi mbalimbali wanaendeela na mapambano ya maambukizi ili kutoka katika hiyo asilimia na kuongeza kuwa Dar es Salaam bila VVU inawezekana pia alichukua fursa hiyo kuwaomba wanaume kujitokeza katika kupima VVU kwani ndiyo kundi ambayo lipo nyuma sana katika kutaka kujua hali zao sambamba na hilo aliwaomba pia watu wadini mbalimbali kuendelea kuwakumbusha watu wawapo kwenye nyumba za ibada.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa