Machi 08, kila mwaka Dunia inahadhimisha siku ya wanawake Duniani ambapo kauli mbiu ya mwaka huu inasema “kizazi cha haki na usawa kwa maendeleo endelevu; tujitokeze kuhesabiwa”
Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam ndugu Hassan Rugwa aliyemuwakilisha Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa huo Amos Makalla amewataka wananchi kudumisha haki na usawa wa kijinsia ili kuleta maendeleo nchini.
Hayo ameyasema leo Machi 3, 2022 katika siku ya maadhimisho ya wanawake Duniani yaliyofanyika viwanja vya Uhuru Jijini Dar es Salaam.
Rugwa ameeleza kuwa Serikali ya Awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, imejikita katika kuhakikisha ajenda ya haki na usawa inapewa kipaumbele hasa kwa kuwawezesha wanawake kushiriki shughuli mbalimbali za kiuchumi, kiafya na kijamii ili kuleta maendeleo nchini.
Aidha ameeleza Serikali inaendelea kuwezesha wanawake kwa kuwapatia mikopo isiyo na riba kutoka kwenye mikopo ya asilimia kumi ya mapato ya ndani kwa kila Manispaa na amewataka wanawake kutumia fursa hiyo vizuri ili kujikwamua kiuchumi.
Akiendelea kuongea katika maazimisho hayo Rugwa ametoa wito kwa jamii kuwa na utamaduni wa kuthamini bidhaa za kutoka ndani ya Nchi yetu ya Tanzania na amewataka Wajasiriamali kutengeneza bidhaa zenye kukidhi mahitaji ya watumiaji ili kuweza kuimarisha uchumi Nchini.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa