Wakati ujenzi wa madarasa 81 kwa ajili ya mapokezi ya wanafunzi wa kidato cha kwanza kwa mwaka 2023 ukiwa umeanza, wajumbe wa kamati za ujenzi wa miradi hiyo wamepata semina elekezi ya namna ya kuzingatia sheria, taratibu, na miongozo katika utekelezaji wa miradi hiyo.
Akiongea kwenye kikao hicho, Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Dr. Peter Nsanya ameeleza kuwa kamati hizo ndizo zenye wajibu wa kusimamia shughuli zote za ujenzi kuanzia ngazi ya kumpata fundi, kununua vifaa na ujenzi wa mradi, hivyo ni vema kila mmoja akafahamu taratibu, kanuni na miongozo katika kutekeleza Majukumu hayo.
Nsanya amewakumbusha wanakamati kutekeleza miradi hiyo kwa wakati na kuzingatia viwango vya ubora kulingana thamani ya fedha.
Aidha, wajumbe hao wamekumbushwa kujiepusha na vitendo vya rushwa katika manunuzi ya vifaa na hatua zingine za ujenzi.
Ujenzi wa madarasa 81 yatatumiwa na wanafunzi 4050 wanaotarajiwa kujiunga na kidato cha kwanza kwa mwaka 2023
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa