Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe. Kheri James akiimbatana na kamati ya Ulinzi na usalama amefanya ziara ya kukagua ujenzi wa madarasa 5 katika shule ya sekondari Saranga na kibamba ikiwa ni kati ya shule 10 zilizopata fedha za ujenzi wa vyumba vya madarasa ikiwa ni maandalizi ya kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka 2023.
Katika Ziara hiyo iliyofanyika Oktoba 19, 2022, Mhe. James alisema kuwa kamati ya ulinzi na usalama imeamua kufanya ziara hiyo ili kujionea utekelezaji wa ujenzi wa madarasa hayo kwani muda wa utekelezaji wa ni mfupi hivyo ni mhimu kufanya ufuatiliaji wa karibu ili kuhakikisha madarasa hayo yanakamilika kwa wakati.
Akiongea baada ya kukagua miradi hiyo, Mhe. James alisema kuwa ameridhishwa na maandalizi ya ujenzi wa Madarasa hayo na amesisitiza kuzingatia ubora pamoja na thamani ya fedha ili kuleta ufanisi na tija katika miundombinu hiyo muhimu kwa maendeleo ya Elimu
Mhe. James ameeleza kuwa fedha za ujenzi wa vyumba hivyo vya madarasa zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ambapo Wilaya ya Ubungo imepokea kiasi cha Shilingi Bilioni 1.62 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 81 kwenye shule 10 za sekondari
Ujenzi wa Madarasa shule ya Sekondari Saranga
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa