- Madiwani kutoka Halmashauri ya Manispaa Ubungo pamoja na wataalamu mbalimbali leo jumatatu Oktoba 31, 2021 wamefanya ziara katika halmashauri ya Manispaa Kahama kwaajili ya kujifunza mambo mbalimbali yanayohusu ukusanyaji wa mapato pamoja mikopo ya asilimia kumi inayotokana na mapato ya ndani ya Halmashauri
- Ziara hiyo maalumu ya kujifunza ambayo imeongozwa na Mstahiki meya wa Manispaa ya Ubungo Mhe. Jaffary Juma Nyaigesha imekua ni ziara yenye mafanikio kutokana na mambo mbalimbali ambayo madiwani hao pamoja na wataalamu wamejifunza
- Aidha Mkurugenzi mkuu wa Manispaa ya Kahama Ndugu Anderson Msumba amepokea vizuri ziara hiyo kisha akaongoza kikao maalumu ambacho kililenga kutoa mikakati mbalimbali ya namna ambavyo Manispaa ya Kahama inaendesha shughuli za maendeleo ikiwemo ukusanyaji wa mapato pamoja na miradi ya maendeleo. Akizungumza katika kikao hicho, Msumba amesema kuwa Manispaa ya Kahama inatarajia kukusanya mapato ya shilingi bilioni Tisa kwa mwaka huu wa wa fedha 2022 - 2023 kutoka kwenye vyanzo vya ndani hasa ikiwa ni ushuru wa huduma
- Msumba ameendelea kusema kuwa katika kuwawezesha wananchi kiuchumi kupitia mapato ya ndani ambapo kutoka mwala 2016 mpaka 2022 Manispaa imetumia Bilioni 5.4 kwenye mikopo hiyo na deni lililopo ni shilingi milioni 495. Kubwa ameeleza juu ya kuandaa mazingira wezeshi ya kazi kwa vikundi hivyo ili vifanye kazi na kurejesha mapema mikopo hiyo. Bwana Msumba ametoa mfano kuwa karibu samani zote za ofisi ya manispaa Kahama zimetengenezwa na wajasiriamali waliofadika na mikopo ya asilimia 10
- Pia katika suala zima la kuwajengea wafanyabiashara wadogo mazingira mazuri ya biashara, Msumba amesisitiza sana suala la ushirikishwaji wa Wananchi ili wawe sehemu ya maamuzi. Manispaa ya Kahama imetenga maeneo maalumu ya wafanyabiashara wadogo ambapo mchakato wake wa kukubalina iliwachukua takribani miaka minne
- Akiongea baada ya ziara hiyo Mstahiki Meya wa Ubungo Mhe. Jaffary Nyaigesha ameeleza kuwa wamefurahishwa sana na mikakati ya maendeleo ya Manispaa Kahama na wamechukua mafunzo hayo na kuahidi kwenda kuyatekeleza kwa vitendo
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa