Baraza la Madiwani Manispaa ya Ubungo limewata wataalamu wa Manispaa hiyo kuhakikisha miradi inayotekekezwa inakamilika kwa wakati ili iweze kuwanufaisha wananchi na kutatua kero mbalimbali.
Baraza limetoa kauli hiyo kwenye mkutano wake uliofanyika tarehe 5 Mei, 2021 kwa ajili ya kujadili taarifa za utekelezaji wa shughuli mbalimbali zilifanyika Kwa kipindi cha mwezi januari hadi Machi mwaka huu na kueleza kuwa wataalamu lazima kuzingatia muda wa utekelezaji wa miradi ili ilete tija kwa wananchi
Waheshimiwa madiwani wakijadili jambo kwenye mkutano wa Wakey wa idea
Wakichangia kwa nyakati tofauti, Madiwani hao wamesema kuwa miradi ikikamilika Kwa wakati inasaidia kusogeza karibu huduma kwa wananchi na kuondoa kero kwa wananchi.
Manispaa ya ubungo inatekeleza miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa Hospitali ya Wilaya na upanuzi wa Hospitali ya Sinza na kituo cha afya kimara miradi ambayo ipo hatua mbalimbali za utekelezaji.
Aidha katika Baraza hilo, wajumbe pamoja na ukusanyaji wa mapato kufikia asilimia 77 hadi mwezi Machi mwaka huu, wamesitiza menejimenti kuongeza kasi ya ukusanyaji wa Mapato pamoja na kubuni vyanzo vipya vya mapato kwani mapato ndio yatawezesha Manispaa kuboresha Huduma mbalimbali Kwa wananchi ikiwemo utekelezaji wa miradi ya maendeleo
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa