- Leo Oktoba 26, 2022 idara ya maendeleo ya jamii Manispaa ya Ubungo imefanya kikao na madiwani wa Halmshauri hiyo juu ya mfumo mpya wa usajili wa vikundi na usimamizi wa mikopo ya asilimia 10 inayotokana na mapato ya ndani ya Halmashauri
- Katika kikao hicho Mkuu wa idara ya Maendeo ya jamii Manispaa ya Ubungo Ndugu Rose Mpeleta amesema kuwa mfumo huo ni mpya ambao umeandaliwa na wizara ya TAMISEMI ili kutatua changamoto mbalimbali za marejesho. Wanakikundi wanatakiwa kutembea kiunganishi cha mikopohalmashauri.go.tz ili kusajili vikundi vyao katika mfumo
- Nae Afisa tehama anayehusika na usimamizi wa mfumo huo kwa Manispaa ya Ubungo ndugu Aziza Lota amesema kuwa mfumo huo utasaidia kusajili vikundi katika namna bora zaidi na pia utarahisisha ufuatiliaji wa marejesho kwa vikundi vitakavyopatiwa mkopo ambapo marejesho yao sasa watakua wanayafanya kwa kutumia namba za kumbukumbu (control number) watakazopewa na ofisi ya Maendeleo ya jamii Manispaa ya Ubungo
Mpaka sasa vikundi ambavyo vimeingia kwenye mfumo kwaajili ya kujisajili ni vikundi 286 ambapo vyeti 211 vimeshachukuliwa na vikundi husika
Aidha kwa vikundi ambavyo bado havijajisajili kwenye mfumo vinatakiwa kufika kwenye ofisi za kata na kuonana na afisa maendeleo wa kata ambaye atawasaidia kwenye zoezi zima la usajili, pia watembelee ukurasa wa Youtube wa UBUNGO MANISPAA kisha watafute "Jinsi ya kusajili kikundi kwenye Mfumo" hapo watapata video yenye maelezo yote kuanzia mwanzo mpaka mwisho wa hatua za usajili
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa