Baraza la madiwani la Halmashauri ya manispaa ya Ubungo limejadili na kupitisha Taarifa za Hesabu za Mwisho za manispaa hiyo kwa mwaka wa fedha 2021/2022 kwenye mkutano maalumu uliofanyika leo Alhamisi Septemba 29, 2022 ikiwa ni utekelezaji wa sheria mbalimbali za fedha za Umma.
Ripoti hiyo imejumuisha taarifa ya mizania, taarifa ya mapato na matumizi, taarifa ya mtiririko wa fedha, taarifa ya mabadiliko ya mtaji na maelezo kuhusu Halmashauri na ripoti hiyo ndiyo itakayopelekea Halmashauri kupata hati safi au mbaya
Katika mkutano huo, baada ya majadiliano Waheshimiwa Madiwani wameruhusu Mchakato wa ufungaji wa Ripoti za Hesabu za Mwisho za Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2021/2022 zilizoishia Juni 30, 2022 uendelee kwa ajili ya kuwasilisha katika Ofisi ya Ukaguzi Mkuu Serikali (CAG).
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa