Madiwani wa Manispaa ya Ubungo wameridhia Sheria ndogo mpya za halmashauri hiyo baada ya kusainiwa na mamlaka husika tayari kwa matumizi katika kutekeleza shughuli mbalimbali za maendeleo ikiwemo sheria ndogo ya afya na usimamizi wa mazingira.
Madiwani wameridhia kutumika kwa sheria ndogo hizo januari 20, 2023 kwenye mafunzo ya kupata mrejesho wa kusainiwa kwa sheria hizo ili kuwa na ufahamu wa kuanza kutumika katika maeneo yao.
Akiwasilisha sheria ndogo hizo Mkuu wa kitengo cha huduma za sheria wa manispaa hiyo Kissa Mbila amesema kuwa kitengo kimeona ni vema kuwasilisha mrejesho wa sheria hizo kwa waheshimiwa madiwani ili wazipokee na kuzifahamu kabla hazijaanza kutumika.
Kissa alieleza kuwa "Najua Madiwani mlishiriki kwenye mchakato wa utungaji wa sheria hizi lakini tumeona busara kuleta mrejesho huu ili mfahamu lakini pia kuridhia matumizi yake mkiwa kama viongozi na wasimamizi wa Halmashauri"
Akianisha sheria hizo zilizotangazwa kwenye tangazo la serikali la tarehe 15 Julai, 2022, Kissa ametaja sheria ndogo 4 ikiwemo sheria ndogo za afya na usimamizi wa mazingira GN Na 495, sheria ndogo za ada na ushuru GN Na 498, sheria ndogo za ushuru wa huduma GN Na 497 na sheria ndogo za vituo vya mabasi na maegesho ya vyombo vya moto
Wakiongea baada ya kuridhia sheria kuanza kutumia Madiwani wamepongeza kitengo cha sheria kufanya mafunzo hayo na kupendekeza kuanza mchakato wa kufanya marekebisho ya baadhi ya vifungu ili viwe rafiki kwa wananchi wa Ubungo.
Ili kuzifahamu kwa undani sheria hizo tembelea kwenye Tovuti ya Halmashauri www.ubungo.go.tz
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa