Madiwani Manispaa ya Ubungo kupitia baraza la kawaida madiwani la robo ya kwanza 2022/2023 kwa nyakati tofauti wameipongeza timu ya menejimenti ya Manispaa hiyo ikiongozwa na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Bi. Beatrice Dominic kwa kufikia lengo la ukusanyaji wa mapato kwa makisio ya robo kwanza ya mwaka 2022/2023.
Hayo yamejiri kwenye baraza la kawaida la Madiwani la robo ya kwanza ya mwaka 2022/2023 ambalo hupitia na kujadili utekelezaji wa taarifa mbalimbali za halmashauri hiyo.
Akiongea wakati anasoma taarifa ya Kamati ya Fedha na Utawala Mhe. Ismail Mvungi kwa niaba ya mwenyekiti wa Kamati hiyo ameeleza hadi kufikia tarehe 30 Septemba, 2022 halmashauri iliweza kukusanya Mapato ya ndani yenye jumla ya Shilingi Bilioni 7.8 ambayo ni sawa asilimia 25 ya lengo la makisio mwaka ya Kufikia shilingi Bilioni 32.
Aidha, Mhe. Mvungi ameendelea kufafanua kuwa kwa kutumia mapato ya ndani ya halmashauri iliweza kutumia Tsh milioni 195.4 kwa ajili ya michango ya mikopo ya asilimia 10 kwa wanawake, vijana na wenye ulemavu na Tsh Bilioni 2.3 imetumika kwenye utekelezaji wa miradi mbalimbali ya halmashauri kwa kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka wa Fedha 2022/2023.
Nae Mhe. Jaffary Nyaigesha Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo amewataka watumishi wa Manispaa hiyo kusimamia vyema ukusanyaji wa mapato kwa vyanzo vyote vya manispaa hiyo.
Pia, Mhe. Nyaigesha amemshukuru Mhe. Rais wa awamu ya sita Samia Suluhu Hassan kwa mgao wa Tsh Bilioni 1.62 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa vyumba 81 vya madarasa kwa shule 10 za Sekondari za Manispaa kwa ajili ya mapokezi ya wanafunzi wa kidato cha kwanza kwa mwaka 2023.
Mhe. Nyaigesha amewataka watumishi wa Manispaa hiyo kuendelea kusimamia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na manispaa hiyo kwa maslahi ya wananchi wa Manispiaa hiyo na Tanzania kwa ujumla.
#ubungoyetufahariyetu
#ubungoyakibingwa
#ubungoupdates
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa