Baraza la Madiwani Manispaa ya Ubungo limetaka kasi kubwa ielekezwe kwenye ukamilishaji wa miradi ya maendeleo na ukusanyaji wa mapato ili Halmashauri iendelee kupata hati Safi na kushika nafasi ya kwanza katika ukusanyaji wa mapato.
Hayo yamesemwa leo tarehe 12/8/2022 kwenye mkutano wa kujadili utekelezaji wa shughuli za maendeleo kwa kipindi cha robo ya nne na kusisitiza kuwa mapato yakikusanywa kwa wingi miradi ya maendeleo itatekelezwa kwa kiasi kikubwa na kwa wakati na hivyo kuboresha huduma kwa wananchi.
Wajumbe wa baraza hilo waliendelea kusisitiza kubuni vyanzo vipya vya mapato kwa ajili ya kuongeza mapato na kwa vile vilivyopo Viendelee kusimamiwa vizuri.Aidha, Wajumbe, waliisitiza Halmashauri kupitia wataalam wake na kamati ya Kudhibiti Ukimwi waweze kusimamia vyema bajeti yakusaidia na kuwahudumia watu walioathirika na maambukizi ya UKIMWI
Nae, Mstahiki Meya Jaffari Nyaigesha alisisitiza wananchi kushiriki katika zoezi la Sensa ya watu makazi linaloenda kufanyika tarehe 23 agosti,2022
Pia amewataka wajumbe kushiriki katika tamasha la Sensa ya Watu na Makazi kwa Wilaya ya Ubungo litakalofanyika Agosti 20,2022 katika viwanja vya Barafu - Mburahati
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa