Mafunzo elekezi kwa wakusanya taarifa za Anwani za Makazi (Data collectors) na watendaji wa Mitaa (90) iliyopo Manispaa ya Ubungo wamepewa elimu kuhusu uhakiki wa taarifa ambayo yamefunguliwa rasmi Leo tarehe 30.6.2022 yakilenga kuhamasisha uchapakazi, weledi katika kazi na uzalendo
Akifungua mafunzo hayo Afisa utumishi Manispaa ya Ubungo Selemani kateti amewataka wahusika katika zoezi hilo kuhakikisha wanazingatia kufanya kazi kwa maadili na pia kuongeza ufanisi ili kufikia lengo
Aliongeza kwa kusema kuwa "Tumelenga kuwatumia nyinyi kwa sababu mlihusika toka kuanza kwa zoezi hili, tuna Imani zaidi mtaenda kulifanya kwa ufanisi zaidi"
Aidha Mratibu wa zoezi la Anwani za Makazi kitaifa Ndg. Jampyon Mbugi Aliendelea kuwasisitiza kuendelea kufanyia kazi zaidi kwani Serikali imewaamini na kuwataka kuendelea kufanyakazi zaidi ya awali na ndo dhumuni la waliotumika katika awamu ya kwanza kurudia katika zoezi hili la uhakiki
Mmoja wa wakusanya Taarifa amewashukuru Manispaa ya Ubungo kupitia wataalam wake ambao wanawapa ushirikiano katika zoezi zima la kuwawezesha kupata mafunzo na kuahidi kwenda kufanya kazi kwa ufanisi ili kufikia lengo.
#UbungoYetuFahariYetu
Attachments area
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa