Mafunzo hayo yametolewa na Mwezeshaji wa mifumo kutoka Ofisi ya Rais-TAMISEMI Ndg.Deogratus Charles Nyati na kufunguliwa na mwakilishi wa Mkurugenzi ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya jamii Manispaa ya Ubungo Rose Mpeleta katika ukumbi uliopo Ofisi ya mkuu wa Wilaya Luguruni.
Dhumuni la mafunzo hayo ni kubaini namna bora ya kufuatilia na kusimamia madai na madeni mbalimbali ya watumishi yasiyokuwa ya mishahara.
Aidha faida za kutolewa kwa mafunzo hayo ya madeni management Information system(MadeniMIS) ni kupunguza malalamiko ya watumishi na kuongeza maadili na ufanisi katika kazi.
Sambamba na hayo Mwezeshaji alisema kuwa mafunzo hayo ni agizo la Mhe.Rais wa awamu ya tano Dr.John Pombe Magufuli siku ya Mei Mosi mwaka huu utengenezwe mfumo ambao utakusanya madeni ya watumishi na kwa sasa serikali inaendelea kushughulikia madeni halali yakiwepo ya walimu ambayo tayari yameshaanza kulipwa.
Nae Mwakilishi wa Mkurugenzi aliendelea kusisitiza kwa wahusika watakao tumia mfumo huo kuwa waadilifu na kuishukuru ofisi ya Rais- TAMISEMI kwa kuwezesha mfumo wa Madeni na madai ya watumishi.
N.B Mafunzo hayo yanafanyika kwa siku mbili na yatamalizika kesho tarehe 18/8/2020
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa