Wawezeshaji wa TASAF katika Manispaa ya Ubungo wamepatiwa mafunzo ya namna ya kufanya uhakiki wa Kaya zinazostahili kupata fedha za TASAF awamu ya tatu sehemu ya pili katika ukumbi uliopo Ofisi ya Mkuu wa Wilaya, Luguruni.
Mafunzo hayo yamezinduliwa na Mwakilishi wa Mkurugenzi wa TASAF ambae pia ni mtaalam wa ufuatiliaji na tathmini Ndg. Fariji Mishael na kuhudhuriwa na Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ambae pia ni Afisa Kilimo Happiness Mbelle, wakuu wa Idara na vitengo na wawezeshaji wa kaya.
Wawasilishaji mada katika mafunzo hayo hayo ni Wakuru C. Nyaratha, Mratibu TASAF Wilaya, Justine Bisangwa, Afisa Ufuatiliaji na Ushauri Wilaya, Dorothy Shiyyo, Afisa Uhawilishaji TASAF Makao Makuu na Sylvia Meku, Meneja wa Takwimu za Jamii kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu.
Wakati akifungua mafunzo Ndg. Fariji aliwataka wakuu wa idara na wawezeshaji kwa ujumla kuwa waadilifu pindi kazi ya uhakiki itakapoenda kuanza.
Aliongeza kuwa zoezi la uhakiki linaenda kufanyika ili kubaini kaya ambazo tunazo kama zinastahili kuendelea kupata fedha za TASAF.
”Kuna baadhi ya kaya zimefanya maendeleo kiasi kwamba ukienda kupima kwa vigezo vilivyopo utagundua wanaweza kuendesha maisha yao, hivyo wanapaswa kuwapisha wale wenye vigezo” Alisisitiza Ndg. Fariji.
Nae Kaimu Mkurugenzi aliwaambia wajumbe kuwa Ofisi ya Mkurugenzi ipo wazi kusikiliza ushauri au kutoa ushauri pale itakapohitajika. Aliongeza kuwa kwa Ubungo uwezeshaji wa TASAF ulikuwa ukifanyika kupitia Manispaa ya Kinondoni lakini kwa sasa Wilaya inajitegemea hivyo hatuna budi kutoa ushirikiano wa kutosha.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa