Wakala wa Barabara Tanzania (TANROAD) Kwa kushirikiana na Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo imefanya zoezi la kuhamisha makaburi 15 yaliyopo Mtaa wa Mbezi kwa Yusufu kata ya Msigani ili kupisha uendelezaji wa mradi wa ujenzi wa barabara ya njia nane.
Zoezi hilo lililofanyika leo Machi 23,2022 limegharimu kiasi cha shilingi milioni kumi na laki tano(10,500,000) kwa ajili ya kulipa gharama ya usumbufu wa kuhamisha makaburi kwa ndugu wa marehemu, kufukua na kuchimba makaburi mapya na gharama za mazishi.
Akitoa ufafanuzi wa utaratibu wa kuhamisha makaburi hayo, Afisa Afya wa Manispaa Boniface Katikiro amesema kila familia imelipwa shilingi laki Tatu (300,000) kama fidia ya usumbufu wa kuhamisha kaburi la ndugu yao.
Amesema kuwa miili ya marehemu 15 imefukuliwa na Kati ya hiyo miili 13 imezikwa katika makaburi ya mshikamano yaliyopo Mtaa wa mshikamano kata ya Mbezi huku miili miwili ikisafirishwa mikoani na ndugu zao.
Akiongea baada ya zoezi hilo Mwenyekiti wa Mtaa wa Mbezi kwa Yusufu Gasper Misibo ameipongezi Halmashauri, TANROAD na ndugu wa marehemu Kwa kufanikisha zoezi hilo kufanyika kwa amani na kupelekea mradi wa ujenzi wa barabara ya njia nane kuendelea kama ilivyopangwa.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa