Naibu Waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi Mheshimiwa Angelina Mabula ameyataka Makapuni ya urasimishaji na upimaji Ardhi katika wilaya ya Ubungo kukamilisha kazi hiyo ipasavyo na kwa wakati ili kuondoa kero ya wananchi ya kutopata hati za umilikishwaji wa ardhi kwa muda mrefu
Mabula ametoa maelekezo hayo Novemba 03,2021 kwenye kikao kazi kilichohusisha makampuni hayo na wataalam wa ardhi wa Manispaa hiyo kutokana na uwepo wa malalamiko kwa wananchi juu ya ucheleweshwaji wa upatikanaji wa hati pamoja na wananchi kuwa wameshalipia gharama za upimaji
"Mnapenda kazi za chapuchapu kwa Kutumia watu wasiohusika, haiwezekani michoro yote ikataliwe lazima kuna shida ikiwemo kupima eneo Mara mbili ili mpate viwanja vingi, hii haikubaliki hatua zitachukuliwa" alieleza Mabula
Pamoja na kuyaelekeza makampuni kutekeleza kazi zao kwa wakati, Naibu Waziri amewaelekeza wataalamu wa Ardhi wa Manispaa ya Ubungo
kuzuia Ujenzi holela katika maeneo mbalimabali kwa kuhakikisha wanajenga baada ya kupata kibali Cha ujenzi.
Ili kupunguza migogoro ya ardhi inayosababishwa na uelewa mdogo wa masuala ya ardhi, Naibu Waziri amewaelekeza wataalam ardhi kutoa elimu kwa wananchi kuhusu Urasimishaji na masuala yote ya ardhi ili wananchi waweze kuwa na uelewa wa kutosha.
Akisoma taarifa ya utekelezaji julai hadi oktoba 2021 Afisa Ardhi Manispaa ya Ubungo Fadhili Hussein amesema kuwa jumla ya migogoro ya Ardhi 171 imepokelewa na migogoro 89 imepatiwa ufumbuzi , migogoro 41 ofisi inaendelea kuitafutia ufumbuzi na 41 inashughulikiwa ngazi ya mahakama
Aliendelea kusema kuwa Halmashauri ilipokea maombi 17 ya wananchi na jumla ya leseni mpya za makazi 14 zilitolewa kwa wananchi na leseni 708 zimelejeshwa kwa matumizi mbalimbali
Vibali vya ujenzi 237 kutoka kwenye maombi 372 vimepitishwa ikiwa ni hatua ya kuhakikisha miji inapangwa inavyotakiwa.
Manispaa ya Ubungo ina jumla ya mitaa 61 ambayo zoezi la urasimishaji unatekelezwa na utekelezaji huo unafanyika kwa kushirikisha makampuni binafsi ya upangaji na upimaji yaliyosajiliwa kwa kujibu wa Sheria
Aidha hadi kufikia mwezi oktoba 2021 jumla ya maeneo 181,390 yametambuliwa, michoro ya mipangomiji 503 yenye jumla ya viwanja 176,350 imendaliwa na kuidhinishwa, aidha viwanja 74,563 vipo katika hatua za awali za upimaji , viwanja 17,776 vimepimwa na kusajiliwa na jumla ya viwanja 3,158 vimeandaliwa hati miliki
2 Attachments
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa