Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Ubungo na Kibamba, Beatrice Dominic amewataka Waongozaji wapiga kura watakaoshiriki katika usimamizi wa Uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba mwaka huu kuzingatia maadili, Sheria, kanuni na taratibu za Uchaguzi ili zoezi hilo lifanyikike Kwa Amani,haki na utulivu.
Rai hiyo imetolewa Leo tarehe 22 oktoba, 2020 na Msimamizi wa Uchaguzi huyo wakati akifungua mafunzo ya makarani hao 4020 yaliyofanyika katika kumbi za mikutano chuo kikuu cha Dar es salaam.
Beatrice amewaeleza kuwa kazi ya karani katika kituo cha kupigia kura inaweza kufanikisha au kuharibu zoezi la uchaguzi hivyo kila mmoja azingatie maelekezo atakayopewa na viongozi wake kwenye kituo cha kupigia kura ili kuondoa malalamiko wakati wa uchaguzi
Pia, Beatrice amewaambia makarani hao kuwa "Serikali imewaamini ndio maana mmechaguliwa kufanya kazi ya ukarani katika Uchaguzi huu, tambueni hatima ya wilaya ya Ubungo iko mikononi mwenu"
Makarani wamesisitizwa kuzingatia viapo vyao vya kutunza Siri za uchaguzi na tamko la kutokuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa ili wasiwe na upendeleo Kwa chama fulani.
Makarani waogozaji wapiga kura majimbo ya Ubungo na Kibamba wakipata maelekezo kuelekea uchaguzi Mkuu oktoba, 2020
Aidha Msimamizi wa Uchaguzi amewaelekeza makarani hao kuwa "Siku ya uchaguzi karani wa kituo hautaruhusiwa kuvaa mavazi ya chama chochote cha siasa kwani mumeapa kujitoa kwenye ufuasi wa vyama vya siasa siku ya uchaguzi"
Makarani wamesisitizwa kuwa kazi wanayoenda kufanya inahitaji ustahimilivu, unyenyekevu na kauli nzuri kwa wapiga kura ili kufanikisha zoezi kwa amani na utulivu kwa kuwaongoza wapiga kura kuingia katika chumba cha kupigia kura.
Manispaa ya Ubungo ina jumla ya vituo 1545 vya kupigia kura katika Uchaguzi mkuu wa mwaka huu kwa jimbo la Ubungo na Kibamba.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa