Tarehe 29/2/2020 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo kupitia Idara ya Afya imeadhimisha siku ya Afya (Afya day) katika viwanja vya chuo cha Ardhi.
Maadhimisho hayo yamekuwa ni kilele cha tathmini ya utendaji kazi wa nusu mwaka kwa idara ya Afya kwa mwaka wa fedha 2019/2020.
Waliohudhuria kwenye shughuli hiyo ni watumishi wa Idara ya Afya wakiongozwa na Mganga Mkuu wa Wilaya Dr. Peter Nsanya , Mwenyekiti wa Bodi ya Afya wa Wilaya, Ndg. Sosthenes Israel, Mbezi Fitness ambao ndio waliowapa mazoezi watumishi, Lancet Laboratories na baadhi ya watumishi wa idara nyingine.
Bonanza hilo la Afya day limeenda sambamba na michezo mbali mbali kama riadha, mpira wa miguu, mpira wa wavu, netball, kukimbiza kuku, ambapo washindi wa michezo yote walipewa zawadi.
Aidha Idara ya Afya ilimzawadia Mkurugenzi kwa kuwa mstari wa mbele katika kusaidia Idara ya afya bega kwa bega na pia imetoa zawadi kwa watumishi wake bora.
Mwisho Mganga Mkuu aliwashukuru watumishi wote kwa kuhudhuria Bonanza hilo kwani michezo na mazoezi inasaidia kupunguza magonjwa yasiyoambukiza.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa