Mkurugenzi Manispaa ya Ubungo Beatrice Dominic amewapongeza Vijana 104 waliofanikiwa kupata nafasi ya ukarani ya ukusanyaji ushuru na kuwataka kufanya kazi ipasavyo ili kuongeza mapato ya Halmashauri
Mkaonyeshe uwezo wenu, mmeaminiwa na serikali mkafanye kazi kwa uweredi. Alieleza Beatrice
"Mkatekeleze majukumu yenu ni marufuku kujitajirisha na fedha za serikali, mkawe waaminifu "
Mmoja wa Vijana hao sitty msafiri amemshukuru mkurugenzi kwa kufaniki kupata ajira hiyo na kuahidi kwenda kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi
Manispaa ya Ubungo imefanikiwa kuajiri Vijana 104 ambao wamefanikiwa kupata ajira ya ukusanyaji ushuru na usafi katika masoko , stendi ya Mabasi ya Magufuli na stendi ya Mabasi Sim 2000
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa