Katika Ukumbi wa TUNU uliopo Mbezi Manispaa ya Ubungo kupitia Idara ya Maendeleo ya Jamii ikiongozwa na Afisa Maendeleo ya Jamii anayeshughulikia dawati la Jinsia Bi. Anita Makota na maafisa Maendeleo wengine.
Akifungua kikao Bi. Anita Makota aliwaeleza wadau hao ambao hushughulika na masuala yanayohusu wanawake kuwa kikao kina nia ya kuja na wazo moja la namna Wilaya ya Ubungo itakavyoadhimisha siku ya wanawake duniani kiutofauti.
“Niiombe jamii na wataalam kutambua thamani na mchango wa mwanamke na tushirikiane sote katika kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto“* aliongeza Mratibu.
Baada ya majadiliano Manispaa na wadau hao wa Asasi za kiraia walikubaliana kuunda “Task Force” ili waweze kuja na wazo la pamoja juu ya namna bora ya kuadhimisha siku hiyo kiwilaya ili iweze kufanyiwa kazi kwa makubaliano ya kufanya kikao cha mwisho kabla ya siku ya tukio.
Baadhi ya wadau walioshiriki ni *Network for Social Education (NESE), World Interaction and Social Progress Organization, Mpakani Tunaweza Organization, Nyota Njema Development Group* na wengineo.
Akifunga kikao hicho Mratibu wa Asasi za kiraia (NGO's) Manispaa ya Ubungo *Bi. Juliana Kibonde* aliwaomba wadau wasiishie kutoa ushirikiano kwa ajili ya siku ya wanawake tu lakini waendelee kushirikiana hata kwenye utendaji kazi wa kila siku.
”Ofisi yangu ipo wazi kwa yoyote atakayekuwa na shida ya miongozo ya kiserikali au hata Asasi nyingine ambazo anaweza kushirikiana katika kazi zao” Aliongeza Juliana.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa