Kikao hicho kilifanyika katika ukumbi wa Tunu Hall uliopo Mbezi na kuongozwa na Mwakilishi wa Mkurugenzi ambaye pia ni Kaimu mkuu wa idara ya Maendeleo ya jamii Mercy Ndekeno Mratibu wa asasi zisizo za Kiserikali Manispaa ya Ubungo Juliana Kibonde na kuhudhuriwa na wawakilishi wa Asasi mbalimbali zilizopo Manispaa ya Ubungo na Wataalam kutoka katika Manispaa hiyo.
Lengo la kikao hicho ni utambuzi wa asasi ambazo zipo Manispaa ya Ubungo na kutathimini shughuli zinazofanywa na asasi hizo na kutengeneza mpango kazi utakao tumika kwa mwaka 2020/2021
"Ni lazima asasi zifanye kazi zake kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu ambazo zitasaidia katika kuhakikisha mnafanya kazi za kuhudumia wananchi ipasavyo na lengo kutimia, pia mhakikishe mnapata kibali kutoka Tamisemi kitakachosaidia asasi zenu kutambulika." Alisema hayo Juliana Kibonde
"Kazi zikafanyike kwa weledi na mkahakikishe mnasimamia misingi yenu ya kazi ili kufanikisha maendeleo ya asasi zenu na kuleta maendeleo katika Manispaa ya Ubungo"Aliongeza Juliana
Aidha mwakilishi wa dawati la Ukimwi Manispaa ya Ubungo ambaye pia ni kaimu Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Mercy Ndekeno aliwaasa kuhakikisha wanatoa elimu kuhusu magonjwa yanayoikumba jamii kwa sasa na kama watekelezaji wa asasi hizo kuwa mstari wa mbele kuhamasisha jamii kujitokeza kupima magonjwa mbalimbali kama ukimwi, shingo ya kizazi n.k
Pia Mwakilishi wa dawati la vijana Bi.Bupe Mwansasu aliwaomba wahakikishe katika asasi zao wanaendesha mafunzo kuhusu stadi za maisha kwa jamii na kushirikiana na wadau kuanzisha vituo vya ushauri nasaha na kuendeleza vipaji vya vijana walioko katika jamii.
Sambamba na hayo Juliana alizungumzia kuhusu dawati la Mtoto na wanawake ambalo Idara ya Maendeleo ya jamii inashughulika nalo kuhakikisha mtoto anapewa haki zake na mwanamke katika jamii kutambua haki zake na kuepeukana na manyanyaso na ukatili wa kijinsia.
Nae mwakilishi wa asasi ya Family Walfare Foundation Angela Mfinanga ameshukuru kwa elimu waliyoipata na maandalizi yaliyofanyika ya kikao hicho.
Mwisho Mercy Ndekeno aliwashukuru kwa ujio wao na kuwakaribisha tena Manispaa ya Ubungo.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa