Manispaa ya Ubungo imekutana na wakandarasi mbalimbali ikiwa ni hatua ya kuanza maandalizi ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa vyumba vya madarasa 151 kwa shule za Sekondari katika Manispaa hiyo kupitia mgao wa fedha zilizotolewa na Mheshimiwa Rais wa Jamuhuli ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan Kwa ajili ya kumaliza changamoto ya upungufu wa madarasa
Ujenzi wa vyumba hivyo 151 utawezesha wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga kidato cha Kwanza Kwa mwaka 2022 kuwa na mazingira mazuri ya kujifunzia.
Akiongea wakati wa kufungua kikao hicho Oktoba 18,2021 Mkurugenzi wa Manispaa ya hiyo, Beatrice Dominic amesema kuwa lengo la kikao hicho ni kuweka mpango Mkakati wa pamoja wa kuanza ujenzi wa madarasa hayo mapema iwezekanavyo ili kufikia mwezi desemba nyumba vyote viwe vimekamilika.
"Ninyi ni wadau muhimu Sana, Nawaomba tushirikiane katika utekelezaji wa mradi huu kwani najua uwezo na utaalamu mnao mfano mzuri tuliweza kujenga madarasa 9 shule ya Msingi king'ongo ndani ya mwezi mmoja, nina amini tukishirikiana tunaweza kukamilisha ujenzi huu kwa wakati kwani fedha zitakuwepo" alieleza Beatrice.
Aidha Beatrice amemshukuru Mheshimiwa Rais kwa kutoa fedha shilingi bilioni 3.02 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 151 kwa shule za Sekondari
"Kwa maeneo yote ambayo miradi hii inatekelezwa, Beatrice ametoa wito Kwa wananchi wa maeneo hayo kutoa ushirikiano kwa wakandarasi watakaopagwa kwenye maeneo yao ikiwemo kuhakikisha vifaa vya ujenzi haviibiwi" alieleza Beatrice
Akiongea kwa niaba ya wa wakandarasi wenzake waliohudhuria kiako hicho Milton Joseph amesema kuwa wanaishukuru Serikali kwa kuwamini tena wakandarasi kutekeleza miradi ya maendeleo tuna ahidi kuifanya kazi hiyo kwa uadilifu na weledi mkubwa ili kuionesha Serikali kuwa tunaweza kujenga Kwa viwango vinavyotakiwa na kwa wakati
Aidha, Wakandarasi wameishukuru Manispaa Kwa kuona umuhimu wa kukutana nasi Kwa lengo la kuweka mikakati ya pamoja namna ya tutafanikisha kazi hiyo kwa wakati, urahisi na ufanisi mkubwa.
"Tamko rasmi la Mheshimiwa Rais kuamuru wakandarasi wahusike kujenga madarasa haya Badala ya mfumo wa zamani wa "Force account" ni hatua kubwa Sana kwetu Kwa sababu ni muda sasa wakandarasi walikuwa hawahusishwi kwenye utekelezaji wa miradi ya Maendeleo" alisema Joseph
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa