Manispaa ya Ubungo imeendelea kusimamia usafi katika mazingira yake hususani kwenye masoko ambako uzalishaji wa taka ni mkubwa sana na hivyo Manispaa imekuwa ikijitahidi kuzoa taka hizo Kwa wakati
Akizungumza wakati wa uzoaji taka katika soko la SIMU2000, Mkuu wa Hifadhi ya Mazingira na Usafishaji Lawi Bernard amesema Manispaa ya Ubungo ina jumla ya magari 3 na mtambo 1 kwa ajili ya kuondoa taka kwenye maeneo ya masoko ikiwemo soko la mbezi, Mabibo gameti, manzese na simu2000 pamoja na maeneo mengine ya umma
Bernard amesema kuwa magari ya kuzoa taka katika masoko makubwa unafanywa kwa wastani wa mara tatu kwa wiki na hii ni kutokana na masoko hayo kuzalisha taka nyingi zinazotokana na bidhaa zinazoharibika kwa haraka hususani matunda.
Zoezi la kuzoa taka katika soko la SIMU2000 leo tarehe 28 januari, 2021
Uzoaji wa taka wa mara kwa mara kwenye masoko na maeneo mengine umesaidia kwa kiasi kikubwa kufanya maeneo mengi ya Manispaa kuwa masafi hususani kwenye masoko ambako uzalishaji wa taka ambazo zinaweza kusababisha harufu mbaya ni mkubwa na hivyo kuleta kero kwa wananchi.
Kwa upande wa maeneo ya barabara na viunga Manispaa inafanya usafi Kwa kutumia wakandarasi ambapo Kwa sasa kampuni ya SUMAJKT ndio inayofanya kazi hiyo
Na hii inahusisha kipande cha barabara ya morogoro kinachopita ndani ya Manispaa, barabara ya Sam nujoma, Mandela, barabara ya Goba na barabara nyingine zinazoozunguka Manispaa
Aidha, taka zinazozalishwa kwenye makazi ya watu Manispaa imeingia mikataba na wakandarasi Kwa kila mtaa Kwa ajili ya kukusanya taka hizo
Magari huwa yanazunguka kwenye Mitaa kulingana na mikataba na ratiba zilizopo kwenye Mitaa hiyo"
Gari la kuzoa taka likipita mtaani kukusanya taka
Akiongea kwa niaba ya wafanyabiashara wa soko la SIM2000 Aisha Juma amesema kuwa anaishukuru na kuipongeza Manispaa ya Ubungo Kwa kusimamia vyema kazi ya uzoaji taka katika soko hilo.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa