Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo imeingia mikataba na kampuni tatu za usafi na moja ya ulinzi ambapo zoezi hilo limefanyika katika ofisi za Manispaa zilizopo Luguruni mbele ya Mkurugenzi wa Manispaa Beatrice Dominic.
Kampuni hizo ni ENGO ENTARPRISES itakayofanya usafi na kuhudumia Makao Makuu ya Manispaa, Kampuni ya JUHUDI CORPORATION COMPANY LIMITED itakayofanya usafi wa barabara kutoka Shule ya Msingi Muhalitani hadi barabara ya Shekilango na barabara ya Mbokemu ( kutoka makutano ya barabara ya Morogoro hadi Sweetcorner- mlandizi road, kwenda Dampo la taka Pugu Kinyamwezi, Kampuni ya CESAM GENERAL SUPPLIES CO. LTD itakayofanya usafi katika barabara ya Sam Nujoma mpaka kiwanda cha Nida.,SENGO 2000 (T) LTD itakayotoa huduma ya Ulinzi Makao Makuu.
Aidha wakati akiwasainisha Mikataba hiyo Mkurugenzi Beatrice Dominic amewataka kufanya kazi kwa kufuata mikataba yao, na alisisitiza kuwa si jambo jema kukiuka masharti hali hii husababisha malalamiko yasiyo ya msingi. Pia amewasihi kuomba malipo kwa wakati na yawe halisi na kuwaasa wawe waadilifu na wafuatiliaji wa watumishi wao.
Lengo kuu la kusaini Mikataba hiyo likiwa ni kuhakikisha Mazingira ya Manispaa ya Ubungo yanakuwa katika hali ya usafi.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa