Manispaa ya Ubungo jijini Dar Es Salaam imeweka mikakati madhubuti ya kuongeza ukusanyaji wa mapato ya manispaa hiyo kwa kuongeza juhudi za usimamizi wa vyanzo vilivyopo pamoja na kubuni vyanzo vipya vya mapato lengo ikiwa kupandisha mapato kutoka bilioni 18 mpaka kufikia angalau bilioni 20 kwa mwaka.
Mikakati hiyo imejadiliwa leo kwenye kikao cha kujadili namna bora ya kuongeza makusanyo ya mapato ya manispaa hiyo kilichojumuisha waheshimiwa madiwani , wakuu wa idara na vitengo pamoja na watendaji wa kata na mitaa ambapo kila kata imewasilisha mikakati ya namna ya kuongeza mapato kwa kuimarisha vyanzo vya mapato.
Wajumbe wakifuatilia majadiliano ya namba ya kuongeza mapato ya manispaa ya Ubungo
Akizungumza wakati akifungua kikao hicho, Mustahiki Meya wa Manispaa hiyo Jaffary Nyaigesha amesema kuwa Manispaa ya Ubungo ina uwezo wa kukusanya mapato makubwa zaidi kuliko inavyokusanya sasa ikiwa tu viongozi na watendaji wa manispaa tutashirikiana kwa pamoja kusimamia ukusanyaji wa mapato.
Mtahiki Meya ameeleza kuwa, Vyanzo vya mapato vinavyotakiwa kusimamiwa ni pamoja na vibali vya Ujenzi, Kodi za ardhi, ushuru wa huduma, kuimarishwa ukusanyaji wa mapato kwenye masoko pamoja na kutengeneza mazingira mazuri ya kufanyia biashara kwa ajili ya kuvutia uwekezaji,ukuaji wa biashara ndogondogo na za kati na hatimaye kuongeza mapato.
Mheshimiwa Diwani wa Kata ya manzese akitoa mchango wa namna ya kuboresha ukusanyaji wa Mapato ya manispaa ya Ubungo.
“Manispaa ya Ubungo inapoteza mapato mengi sana kutokana na mianya mingi ya uvujishaji mapato kutokana na usimamizi mdogo au baadhi ya viongozi
Kwa upande wake Diwani wa kata ya Sinza ameeleza kuwa , Pamoja na kubuni vyanzo vya mapato na kusimamia ukusanyaji wa mapato, wajumbe wa kikao wameadhimia kuongeza utoaji wa elimu ya mlipa kodi ili wafanyabiashara watambue umuhimu wa kulipa kodi kwa hiyari “ tumieni vyombo vya habari ikiwemo radio za kijamii pamoja mitandao ya kijamii ambayo imeonekana kutumiwa zaidi kupata taarifa mbalimbali”
Aidha, Mkurugenzi wa Manispaa Beatrice Dominic ameeleza kuwa Manispaa inaendelea kusimamia ukusanyaji wa mapato kwa njia ya kielektroniki ambapo jumla ya PoS 130 zinatumika kukusanya mapato katika vyanzo mbalimbali ikiwa njia ya kuhakikisha mapato ya Manispaa hayapetei, pia Manispaa iko kwenye mchakato wa kununua PoS 100 Kwa lengo la kuimarisha ukusanyaji wa mapato.
Pia, Beatrice amesisitiza watendaji wa kata na Mitaa kusimamia kwa dhati ukusanyaji wa mapato pamoja na kubuni vyanzo vipya vya mapato ili Manispaa isipoteze mapamapato
Watendaji wa kata na mitaa wakisikiliza kwa makini Kikakati ya kuongeza ukusanyaji wa mapato
"Tunapaswa kuwajibika Kwa pamoja ili kuongeza Kasi ya ukusanyaji wa Kodi na tozo mbalimbali ili tuboreshe utoaji wa huduma kwa wananchi ikiwemo utekelezaji wa miradi ya maendeleo" alisisitiza Beatrice
Kwa mwaka wa fedha 2020/2021 Manispaa ya Ubungo ilikasimia kukusanya bilioni 18 na mapaka sasa imefanikiwa kukusanya Zaidi ya 45%.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa