Ikiwa zimebaki Siku chache kufunguliwa kwa shule, Manispaa ya Ubungo leo januari 8, 2021 imekabidho madawati 200 shule za sekondari ambazo zina upungufu wa viti na meza ikiwa ni maandalizi ya kuwapokea wanafunzi wa kidato cha kwanza kwa mwaka 2021.
Akizungumza wakati wa kukabidhi viti na meza hizo, Afisa elimu wa Manispaa hiyo Hilda sharanda amesema kuwa Manispaa imekabidhi viti na meza hivyo 200 kwa shule za sekondari ikiwa ni moja ya mkakati wake wa hukakikisha wanafunzi wa kidato cha kwanza kutoshindwa kusoma kwa sababu ya ukosefu wa viti na meza.
Sharanda ameeleza kuwa, Wanafunzi wote 13, 347 walichaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza watasoma katika mazingira mazuri kwani Manispaa imetoa fedha shilingi milioni 115 kwa ajili ya kutengeneza viti na meza ambapo kwa leo tu akabidhi viti na meza hizi 200 huku vingine 1000 ikiwa hatua za mwisho za matengenezo
Kwa ujumla, shule zina upungufu wa viti na meza 2847 kati ya 10500 vilivyopo ambapo katika upungufu huo viti 1200 vinatengenezwa na Manispaa kupitia mapato ya ndani, 1000 vimefanyiwa ukarabati shuleni hivyo tunaendelea kuomba wadau wengine waendelee kutusaidia ukizingatia elimu ni sekta mhimu sana kwa ustawi wa jamii na Taifa kwa ujumla.
Kwa upande wa vyumba cha madarasa , sharanda amesema kuwa wanafunzi 13,347 waliofaulu kujiunga kidato cha kwanza wanahitaji vyumba cha madarasa 268 lakini vyumba 231 vipo na hivyo kufanya upungufu wa vyumba 37
Aidha, sharanda amesema, katika kukabiliana na upungufu huo manispaa imetoa fedha milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba cha madarasa 37 ambapo utekelezaji wake upo hatua mbalimbali lengo ikiwa ni kuhakikisha wanafunzi wote walichaguliwa kuanza kidato cha kwanza hawaikosi furss hiyo kutokana na ukosefu wa madarasa ya kusomea.
Kutokana na juhudi hizi za Manispaa na serikali kwa ujumla, sharanda amewataka wazazi na walezi wahakikishe wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza wanaripoti shule kwa wakati wakiwa na mahitaji yote ya msingi kwani mazingira ya kujifunzia yako vizuri yaani Walimu, madarasa na madawati.
Akiongea wakati wa kukabidhiwa viti na meza kwa ajili ya kidato cha kwanza Mwalimu Andrea Ndagire kutoka shule ya sekondari Kibweheri ameishukuru serikali kupitia Manispaa ya Ubungo kwa kutoa viti na meza hizo kwani vitapunguza kwa Miesi kikubwa upungufu uliokuwepo shuleni mwaka
Aidha Mwalimu Ndagire ameeleza kuwa kitendo cha Manispaa ya hiyo kutumia fedha nyingi kwa ajili ya kutatua changamoto katika sekta ya elimu ni kutekeleza kwa vitendo Dhana ya uchumi wa kati kwa vitendo maana wanafunzi anakuwa katika mazingira mazuri ya kujifunzia na hivyo kuwa na Taifa bora ukizingatia elimu ni msingi wa ustawi wa sekta zingine.
Walter priscus prosper ni moja ya wanafunzi walichaguliwa kujiunga kidato cha kwanza katika shule ya sekondari kimara, ameipongeza serikali kwa kutoa viti na meza kwenye shule zake ili wanafunzi wasome katika mazingira mazuri.
"Kwa niaba ya wanafunzi wenzangu tunaahidi kusoma kwa bidii ili fedha zinazotumika kujenga miundombinu ya shule pamoja na utoaji wa elimu bila malipo zisipotee bure" aliahidi mwanafunzi prosper.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa