Leo tarehe 23 desemba,2020, Kamati ya Fedha na Uongozi ya Manispaa y Ubungo jijini Dar Es Salaam imetembelea mradi wa nyumba za kupangisha ( apartment) za zilizopo osterbay jijini humo lengo ikiwa ni kuhakikisha chanzo hicho kinakusanya Mapato kama ilivyokusudiwa.
Akiongea baada ya kutembelea nyumba hizo, Mhe. Mbunge wa Ubungo Dkt Kitila Mkumbo ambaye pia ni Waziri wa Uwekezaji ameeleza kuwa, Kamati hiyo ina wajibu wa kusimamia masuala ya fedha ikiwemo kusimamia ukusanyaji wa mapato kwa vyanzo vilivyopo na kubuni vyanzo vipya
Serikali inahimiza Uwekezaji wa miradi mkakati ambayo itaiingiza mapato Serikali "Uwekezaji huu ni mzuri sana kwani mahitaji ya nyumba za kupanga hapa jijini no makubwa nawahimiza tuzitangaze tutapata wapanhaji na hatimaye Manispaa itapata mapato"
Wajumbe wa kamati ýa fedha na uongozi wakikagua nyumba hizo.
Dkt Mkumbo ameendelea kusema kuwa " Naomba nitumie nafasi hii kuwakaribisha watu kuja kupanga katika nyumba hizi kwani zina ubora wa hali ya juu na ziko sehemu nzuri Sana lakini pia kuna huduma zote mhimu ikiwemo sehemu ya kupaki magari viwanja vya michezo pamoja na bwala la kuogelea"
Aidha Kamati imeahidi kushirikiana na wataalam wa Manispaa hiyo kuhakikisha mapato yanakusanywa ipasavyo bila kuacha mianya yoyote ya upotevu wa Mapato.
Wajumbe wa Kamati fedha na uuongozi ya Manispaa ya ubungo wakifanya majadiliano baada ya kukagua mradi wa nyumba za kupangisha zinazomilikiwa na Manispaa hiyo.
Nae Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Beatrice Dominic amesema kuwa , awali Manispaa ailitafuta dalali wa kupangisha nyumba hizo juhudi ambazo hazija zaa matunda ndio maana kwa sasa tumejipanga kuzitangaza zipate wapangaji ili kuiingizia mapato Manispaa kama ilivyopangwa.
Beatrice ameeleza kuwa , Ufuatiliaji huo utafanyika kwenye vyanzo vyote vya Mapato ili kwenda Sambamba na agizo la Serikali la kuzitaka Halmashauri kuongeza ukusanyaji wa mapato ya ndani kwa lengo la kupunguza utegemezi wa fedha kutoka Serikali kwa bajeti ya sasa.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo akitoa maelezo kwa wajumbe wa kamati ya Fedha na uongozi leo tarehe 23.12.2020 ilipotembelea apartment za kupangisha za osterbay Villa.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa