Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla ameipongeza Manispaa ya Ubungo kwa kupata HATI safi Mara nne mfululizo katika ukaguzi wa hesabu za Serikali
Makalla ametoa pongezi hizo Leo juni24,2021 baada ya kupokea taarifa ya mdhibiti na mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali za Manispaa hiyo kwenye baraza maalum la Madiwani la kujadili hoja lililofanyika katika ukumbi wa Manispaa hiyo
"Niwapongeze kwa kupata HATI safi Mara nne mfululizo endeleeni kulinda heshima hiyo kwa kuweka mikakati ya kujibu na kuto kuzalisha hoja zengine" Alisema hayo Makalla
Aidha alisema kuwa Hati safi inamaana kubwa Sana kwa wananchi kwani inawapa imani kuwa Halmashauri haitumii vibaya fedha za Umma hali itakayo saidia wao kushiriki katika shughuli mbalimbali za maendeleo bila vikwazo
Pamoja na hayo Makalla amesisitiza ukusanyaji wa mapato kwa kuzingatia Sheria na kanuni za fedha hususani matumizi sahihi ya vifaa vya kielectroniki(POS)
Pia Makalla ameipongeza Manispaa ya Ubungo kwa kufikia 97% ya makusanyo ya fedha za mapato ya ndani na kusema kuwa juhudi ziendelee ili kufikia asilimia 100 ya makusanyo yake
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Beatrice Dominic alimuahidi RC kutekeleza maagizo yote ikiwemo kujibu hoja ndani ya mwezi mmoja
Kuanzia mwaka 2017/2018 hadi sasa Manispaa ya Ubungo imekuwa ikipata HATI safi mfululizo
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Beatrice Dominic akitoa maelezo leo juni 24, 2021 kwenye baraza maalumu la madiwani la kujadili hoja za mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa