Manispaa ya Ubungo tarehe 25 august 2021 imepokea Baiskeli 22 kutoka shirika la AMREF kupitia mradi wake wa afya kwa ajili ya kurahisisha shughuli za kusafirisha sampuli za makohozi kutoka kwenye jamii kwenda kwenye vituo vyenye mashine za Gene expert kwa ajili ya upimaji wa kifua kikuu
Akiongea wakati wa kupokea baskeri hizo Kaimu Mganga mkuu Allen Kallongola amewashukuru na amesisitiza utunzaji wa baiskeli hizo kwa watumiaji wote waliofanikiwa kupata usafiri huo
Aliendelea kwa kuwaagiza watumiaji wa vifaa hivyo kuhakikisha wanatoa elimu kwenye jamii na kuwafikia wahisiwa wa kifua kikuu ili kuweza kuibua wagonjwa wengi wa kifua kikuu ili kutokomeza kabisa kifua kikuu ifikapo 2030
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa