Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe. KISARE MAKORI na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo BEATRICE DOMINIC leo hii wamewapokea wabunge 2 wa Bunge la CANADA wakiongozana na wajumbe wengine kutoka Nchini CANADA. Wageni hao wamefika Manispaa ya Ubungo lengo kuu likiwa ni kuona matumizi ya vishkwambi (tablets) na chanjo ambazo zinafadhiliwa na shirika la GAVI ambalo Canada ni mdau mmoja wapo wa shirika hilo linalosaidia maswala ya Chanjo Duniani.
Nishukuru kwa ujio wenu na msaada ambao tumeupata kutoka kwenu kwani inaonyesha ni jinsi gani mmekuwa na ukaribu mzuri na ushirikiano wenu kwetu umekua mzuri katika kuleta maendeleo katika zahanati zetu za Wilaya ya Ubungo kwa kutoa vifaa ambavyo vinasaidia wananchi wetu na kuleta maendeleo katika utoaji na upatikanaji wa taarifa kiteknolojia kwa kutumia Vishikwambi (tablet)na chanjo ambazo zinasaidia kwa watoto ambao wapo katika umri wa chini ya miaka mitano kwani inasaidia katika kuleta kizazi chenye afya nzuri kwa taifa”. Alisema Mkuu wa Wilaya.
Nae Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Beatrice Dominic alishukuru kwa ujio wao na msaada ambao wameutoa kwa Wananchi wa Manispaa ya Ubungo kwa kupata mfumo mpya wa utunzaji wa taarifa kwa kutumia Vishikwambi (tablet) na maendeleo kwa ujumla ambayo Zahanati zetu za Manispaa ya Ubungo imepata hasa chanjo ambazo zinafadhiliwa na shirika hilo
Nipende kuwakaribisha tena na sisi kama Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo tutahakikisha wananchi wanapata huduma Bora za afya ili kuondoa umasikini na kukuza uchumi wetu kama lilivyo lengo la serikali ya awamu ya tano. Nia ya halmashauri ni kuhakikisha kuwa misaada inayotolewa na wafadhili hawa inatumika kwa lengo lililokusudiwa na si vinginevyo. Aliongeza Mkurugenzi
Pia Mganga mkuu wa Manispaa ya Ubungo Dk.Peter Nsanya kwa kumalizia alitoa pongezi na shukrani za pekee kwa ugeni uliokuja kwa msaada ambao wameutoa kwani umewezesha maendeleo ya zahanati kwa kusaidia wauguzi kupunguza kazi ya kujaza vitabu pindi mteja anapofika kupata huduma.. Mfumo huo utatoka taarifa sahihi na kwa wakati za chanjo na wateja.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa